FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Thursday, 26 June 2014

PICHA ZA UTATRAAAA ZA MSANII CINDY RULZ NA AMA THE MAKER ZAVUJA YADAIWA WAMEKOLEA KIMAHABA. CHEKI HAPA


Katika pitapita zetu camera ya Bongoclan imefanikiwa kupata picha za utata za msanii Cindy Rulz akiwa na Ama the maker ambaye pia ni msanii. Tukio hilo lilitokea wik iliyoisha katika club moja ya usiku na kuwaacha watu midomo wazi.
Habari tulizozipata kutoka kwa watu wa karibu wa wasanii hao zinasema kua wawili hao wameonekana mara nyingi wakiongozana pamoja karibu kila sehemu hasa katika club za usiku huku wakionekana katika mahaba mazito.
Baada ya kupata taafifa hizo tuliamua kumvutia waya Ama the maker na kumuuliza kuhusu skendo hiyo lakini kwa zaidi ya mara 20 tulizompigia simu hakuweza kupokea simu na bado tunaendelea kutafuta mawasiliano ya Cindy ili na yeye afunguke.


CIndy Rulz ni msanii pekee wa kike anayefanya Hip Hop ambae anafanya vizuri kwa sasa hapa Tanzania huku Ama the maker akiwa anatamba na wimbo wake wa Ulemsoga.

No comments:

Adbox