Lupita
amezidi kuchukua headlines za vyombo mbalimbali vya habari tangu
afanikiwe kuchukua tuzo za Oscar na kutajwa kama mwanamke mrembo zaidi
duniani, sasa amethibitisha kuhusu upande wake wa mahusiano kuwa ni
kweli ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki K’naan kutoka Somalia.
Mara
ya kwanza Lupita alikuwa akihusishwa na Michael Fassbender na Jared
Leto lakini mwigizaji huyo amekita mizizi yake ya kimapenzi kwa rapa
K’naan na wanafuraha na mahusiano yao.
Wapenzi
hao mara kadhaa wamekuwa wakionekana katika maeneo mbalimbali wakiwa
pamoja lakini hawakuwa wakiweka wazi nini kinaendelea kati yao na
kufanya watu wahisi tu juu ya uhusiano wao.
Stori
ni kwamba katika jarida la hivi karibuni la Vogue ambalo Lupita
ametokea kwenye ukurasa wa mbele amethibitisha kweli ana uhusiano wa
kimapenzi na K’naan na anampenda sana.
K’naan
ni mzaliwa wa Somalia na ameingia katika umaarufu baada ya kuimba wimbo
rasmi wa kombe la dunia kwa mwaka 2010 wa “Wavin’ Flag”.
No comments:
Post a Comment