Friday , 27th Jun , 2014
Kiungo
mshambuliaji mpya wa timu ya Young Africans SC Andrey Marcel Ferreira
Coutinho amewasili mchana wa leo jijini Dar es salaam akitokea kwao
nchini Brazil tayari kwa kuanza kazi ya kuwatumikia wana Wanajangwani
katika msimu wa 2014/2015.
Andrey Marcel Ferreira Coutinho akiwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere mchana wa leo
Kiungo
mshambuliaji mpya wa timu ya Young Africans SC Andrey Marcel Ferreira
Coutinho amewasili mchana wa leo jijini Dar es salaam akitokea kwao
nchini Brazil tayari kwa kuanza kazi ya kuwatumikia wana Wanajangwani
katika msimu wa 2014/2015.
Countinho amewasili mchana kwa shirika la Ndege la Afrika Kusini (South African Airways) akitoka jijini Sao Paul ambapo safari ya kuja Tanzania imemchukua takribani masaa 20 tokea katika Mji wa Berem ambapo ndipo anapoishi.
Mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa JK Nyerere, Coutinho alipokelewa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Bw. Mohamed Bhinda ambaye alimuongoza kuwasilimia washabiki na waaandishi wa habari waliojitokeza kumlaki.
Akiongea na waandishi wa habari Uwanja wa Ndege Coutinho amesema anajisikia furaha kuwa Tanzania, nchi ambayo watu wake wanapenda mpira na kikubwa amekuja kuisaidia Yanga kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali itayakayowakabili.
Kuhusu changamoto za ugeni katika Bara la Afrika, Coutinho alisema soka kwake ni kazi, ana uzoefu baada ya kucheza pia Barani Asia hivyo hana wasiwasi, na kwa kuwa na walimu aliowazoea anaamini kwa pamoja atafanya vizuri.
Msafara wa kutoka Uwanja wa ndege ulielekea makao makuu ya klabu mitaa ya Twiga/Jangwani ambapo Coutinho aliwasilimia wapenzi, washabiki na wanachama waliojitokeza kumpokea, kisha aliongea na katibu mkuu Bw Beno Njovu kabla ya kwenda kupumzika.

No comments:
Post a Comment