Diamond Platnumz ni msanii mwingine mkubwa wa Kitanzania aliyejiunga na Mkito.com kwaajili ya kusambaza muziki wake mtandaoni. Msanii huyu anajiunga na wengine kama Fid Q, Nay Wamitego, Rich Mavoko, Vanessa Mdee, Juma Nature, Barnaba, Linah, Belle 9 na wengine wengi katika mchakato unaoendelea kuwawezesha wasanii kujipatia kipato kutokana na muziki wao kupakuliwa kwenye mtandao
Diamond kabla ya kuondoka kuelekea Afrika ya Kusini kwaajili ya video
yake mpya aliona ni vyema kuungana na Mkito.com kwani ni kampuni ya
Kitanzania yenye madhumuni mazuri kwa tasnia ya muziki nchini.
Watumiaji wote wa Mkito.com sasa wanaweza kupata nyimbo za Diamond kupitia www.mkito.com ikiwemo albam ya Best Of Diamond na pia wimbo wake mpya Mdogomdogo



No comments:
Post a Comment