FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Tuesday, 1 April 2014

Urusi yaipandishia Ukraine bei ya Gesi

Ukraine hununua gesi yake nyingi kutoka kwa Urusi
Kampuni ya Gasi nchini Urusi GAZPROM imeongeza bei ya bidhaa hiyo inayoilipisha Ukrain kuanzia hii leo.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Alexei Miller amesema kuwa hatua hiyo inatokana na Ukrain kushindwa kulipa deni lake ambalo linadaiwa kuwa dola billioni moja na nusu.
Urusi imekuwa ikiipatia Ukraini ruzuku ya gesi na sasa taifa hilo linakabiliwa na kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo kwa thuluthi moja.
Serikali ya mpito ya Ukrain inajaribu kufanya kazi chini ya mazingira magumu kwa kuwa haiwezi kufaulu kupewa mkopo na hazina ya shirika la fedha duniani huku bei ya gesi ikitarajiwa kupanda mwezi ujao.
Miller amesema kuwa kampuni ya GAZPROM itaongeza bei ya gesi inayonunuliwa na Ukrain kutoka dola 269 hadi dola 386 katika kila mita 1000 za ujazo.
Bei hiyo inaondoa mapunguzo ambayo aliyekuwa rais wa Ukrain Victor Yanukovych alikuwa amejadiliana na Urusi.
Tangazo hilo la bwana Miller hata hivyo lilitarajiwa kwani maafisa wa Urusi hapo mbeleni walikuwa wamesema kuwa wataongeza bei ya bidhaa hiyo hata kabla ya kuchaguliwa kwa serikali mpya iliyopinduliwa nchini Ukraine.
Urusi imesema serikali mpya ya Ukrain sio halali.
Kwa upande wake Ukrain inalitegemea sana taifa la Urusi kwa gesi.
Serikali ya Urusi imeichukulia hatua kali Ukrain kwa kushindwa kulipa deni la gesi yake huku adhabu ya hivi karibuni ikiwa ile ya mwaka 2009 ambapo Urusi ilikata usambazaji wa gesi nchini Ukrain.
Hatua hiyo iliiyaathiri mataifa mengine ya ulaya ambayo pia yanategemea Urusi kupata gesi.

No comments:

Adbox