Waheshimuni sana WANAWAKE.
Nimegundua kwamba kumdharau mwanamke yoyote yule ni sawa na kumdharau mama yako mzazi kwasababu mama yako nae alikua binti wa kawaida tu kabla hajakuzaa wewe.
Vivyo hivyo huyo mwanamke unayemdharau leo will probably be mama wa FULANI in the near future.
Huyo FULANI anaweza akawa Rais wako, mchungaji wako n.k, bila kujali kwamba amezaliwa(ametoka) kwenye tumbo la mwanamke wa aina gani (malaya au anayejiheshimu). Kitanda hakizai haramu.
Nina ushuhuda...
Dada yangu amejifungua, nilikua nasikiaga tu eti "hakuna kama mama", sasa nimethibitisha.
Hakubahatika kujifungua kwa njia salama, hivyo baada ya kujifungua ameteseka sana na mshono, wakati huohuo halali usiku, mtoto akihitaji kunyonya hata kama ni usiku wa manane anaamka kwa tabu kwasababu ya maumivu makali ya mshono anayoyapata, ila anahakikisha anamnyonyesha au kumbembeleza.
Wakati mwingine mtoto akicharuka halali usiku kucha, namuonea huruma sana ila yeye kwake ni faraja kumuona mwanae kapumzika!
Imefikia kipindi namtazama mama yangu usoni bila kummaliza, kumbe alipata shida zote hizi!
NAWAHESHIMU SANA WANAWAKE WOTE! Maneno haya yanatoka moyoni mwangu.
No comments:
Post a Comment