MTABIRI mwenye jina kubwa kwa sasa Bongo, Maalim Hassan Yahya Hussein ambaye ni mrithi wa kazi za marehemu Yahya Hussein ameibuka wiki hii na kuanika kwamba, Agosti mwaka huu Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Wema Sepetu watafunga ndoa
Akizungumza na Amani jijini Dar es Salaam juzikati, Hassan alisema amepiga mahesabu ya kinyota kwa wapenzi hao na kubaini kuwa, Agosti ndoa yao itafungwa mahali popote nchini Tanzania.
Akaongeza: “Kama wapo kwenye mipango au maandalizi wakazane, kwani mwezi Agosti ndiyo wenyewe kwa mujibu wa nyota za wote
“Lakini nawapa angalizo muhimu, wakae wakijua kwamba kama ndoa hiyo haitatimia Agosti kutokana na sababu zao wenyewe, haitafungwa tena hadi mwaka 2016, kwa sababu lazima ndoa yao iwe kwenye mwaka unaogawanyika.”
No comments:
Post a Comment