FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Thursday, 3 April 2014

JOKATE MWEGELO ADAI BADO YUPO SINGLE TOKA AMEACHANA NA DIAMOND


Jokate Mwegelo yupo single and ready to mingle.. atleast for now. Staa huyo mwenye vipaji lukuki alisema hayo Jumatatu hii kwenye kipindi kipya cha TV1, ‘The One Show’ anachokiendesha kwa kushirikiana na Ezden Jumanne aka The Rocker


Katika kipindi hicho cha kwanza kuoneshwa, watangazaji hao walianza kwa kuhojiana wao kwa wao kwanza na moja ya maswali aliyoulizwa Jokate ni kama yupo kwenye uhusiano wowote wa mapenzi. Jokate ambaye pamoja na kuwa muigizaji wa filamu pia ni muimbaji wa muziki na mjasiriamali, alisema kuwa kwa sasa yupo single lakini haimaanishi kuwa wanaume hawamsumbui kumtaka kimapenzi.

Jokate amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mchezaji wa basketball wa timu ya Oklahoma City Thunder, Mtanzania Hasheem Thabeet pamoja na uhusiano uliodumu kwa kipindi kifupi na staa wa muziki, Diamond Platnumz.

No comments:

Adbox