Habari zilizotangazwa juu ya mawasiliano ya mwisho kati ya wafanyakazi wa Feri iliyozama Korea Kusini na maafisa wa kudumisha usalama baharini zinaonyesha kuwa kulitokea hali ya wasiwasi kabla ya mkasa huo, ambayo huenda ilichangia pakubwa vifo vya abiria wengi katika feri hiyo.
Taarifa hiyo mpya imetolewa jana alasiri wakati ambapo imethibitishwa kuwa maiti 62 zimepatikana kwenye mabaki ya feri hiyo, na kufanya idadi ya watu waliothibitishwa kufariki kufikia 58. Zaidi ya watu 240 hawajulikani waliko hivi sasa.
Mama mmoja alisema kuwa watoto waliofariki walikuwa wakitunzwa vizuri.Jamii za watu ambao hawakuwa wamepatikana walifanya maombi ya Pasaka Jumapili katika chumba cha kufanyia mazoezi katika eneo la Jindo, ambako mamia ya watu wamekusanyika tangu feri hiyo kupinduka wakisubiri habari kuwahusu wapendwa wao.
"Naamini watoto hao wako mbinguni na Mwenyezi Mungu aliyefufuka. Naamini Naamini mimi," mama huyo alisema.
Jung Maria, mwanamke aliyejitolea kuzisaidia familia za walioathirika, alisema kuwa jamaa za watu wasiojulikana waliko wanapaswa kusikia kilichotokea kwa njia moja au nyingine.
"ikiwa wamefariki, tunapaswa kupata miili yao haraka iwezekanavyo. Na iwapo kutatokea muujiza basi turejeshewe watoto hao upesi pia, alisema mfanyakazi huyo wa kujitolea
Idadi kubwa ya abiria katika meli hiyo walikuwa wanafunzi wa shule ya upili waliokuwa wakienda kwenye mojawapo wa kisiwa kubarizi. Hadi kufikia sasa kumekuwa kungali kuna ubishi mkubwa iwapo nahodha mwenyewe alikuwa ameshikilia sukani.
No comments:
Post a Comment