Hivi karibuni Diamond Platnumz atasikika kwenye wimbo wa wasanii wakubwa wa Nigeria, Don Jazzy, Waje na Dr Sid waliomshirikisha kwenye nyimbo zao alipokuwa nchini humo mwezi huu.
Staa huyo amezungumza na Bongo5 kuhusiana na jinsi alivyokutana na wasanii hao.
“Wakati nipo Nigeria nimebakiza siku moja kurudi wakaniemail wakaniambia ‘Mavin Records, Don Jazzy na Dr Sid wangependa kufanya kazi na wewe kama bado upo Nigeria,” Diamond ameiambia Bongo5. “Niliona ni jambo zuri kufanya kwasababu Don Jazzy ni mtu mkubwa na ukiangalia industry ya muziki ni mtu ambaye ana sehemu yake. So nikakaa na uongozi wangu nikawaambia ‘nimepata email kutoka kwa Don Jazzy anasema anapenda kufanya kazi na sisi. Basi nikawa link na menejimenti yangu wakazungumza wakapanga vitu vyote vinavyotakiwa tukaenda tukafanya,” ameongeza.
Amesema katika wimbo huo wa Dr Sid, Don Jazzy ambaye ndiye producer naye ameweka sauti yake. Hata hivyo Diamond amesema wimbo alioshirikishwa na Waje ndio alioupenda zaidi na kwamba utakuwa moto wa kuotea mbali.
No comments:
Post a Comment