FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Tuesday, 22 April 2014

DAVID MOYES KAZI TENA HANA


Vyombo vya habari vya Uingereza, likiwemo Mail on Sunday vimeripoti kuwa David Moyes ataachishwa kazi wiki chache zijazo na kwamba anaweza kuachiswa hata leo au kesho

Wamiliki wa timu hiyo, familia ya Glazer wanadaiwa kuishiwa uvumilivu kwa kocha huyo ambaye tangu aanze kuinoa imeendelea kufanya vibaya na sasa ikiwa nafasi ya saba kwenye msimamo wa Barclays Premier League. Jana Man United ilifungwa mabao 2-0 na Everton.

Uongozi wa juu wa klabu ulikuwa umepania kumpa muda kocha huyo lakini umeona ni ngumu kuona mabadiliko kwakuwa hata wachezaji hawamwamini tena kocha wao. Ripoti hizo zinadai kuwa nafasi yake inaweza ikachukuliwa kwa muda na Ryan Giggs huku makocha wanaowaniwa kuchukua nafasi ya muda wote wakitajwa kocha wa Dortmund, Jurgen Klopp, kocha wa Uholanzi, Louis van Gaal na kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti

No comments:

Adbox