Polisi nchini Nigeria
Inaarifiwa kuwa watu kadhaa
wamekufa na wengi kujeruhiwa katika msongamano kwenye uwanja wa michezo
wa taifa katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja.
Majeruhi kadhaa wamepelekwa hospitali lakini maafisa hawana uhakika watu wangapi wamekufa.Mwandishi mmoja wa habari mfaransa anasema aliona maiti saba.
Hayo yalitokea wakati wa kuajiri watu katika idara ya uhamiaji ya Nigeria.
Maelfu ya watu walijitokeza kufanya mtihani wa ajira - inaarifiwa mkanyagano ulitokea walipojaribu kufika katikati ya uwanja.


No comments:
Post a Comment