FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Monday, 24 March 2014

KUAMBIANA: KIPIGO NILICHOWAPA WEMA SEPETU NA AUNT KIMEWAPA ADABU



Stori: Imelda Mtema

‘DAIREKTA’ na muigizaji wa filamu Bongo, Adamu Phillip Kuambiana amefunguka kuwa kitendo cha kuwatia makofi waigizaji Wema Spetu na Aunt Ezekiel kilikuwa cha kiungwana sababu amewafundisha.

Akipiga stori na paparazi wetu, Kuambiana alisema bila kuwa mkali wakati mwingine mambo huwa hayaendi kwenye uigizaji hivyo anapotembeza kichapo kidogo, mambo yanakwenda katika mstari.

“Kipigo kinasaidia, watoto wa kike hawa bila kuwatishia wanafanya wanavyotaka na ukiwaruhusu unaweza kuharibu kazi,  lakini nashukuru wamenielewa, tunapiga kazi,” alisema Kuambiana.
GPL

No comments:

Adbox