MSANII wa muziki na filamu Bongo, Baby Madaha na meneja wake, Joe
Kariuki wanatarajia kufunga ndoa Novemba, mwaka huu nchini Kenya jijini
Nairobi.
Akizungumza na mapaparazi wetu, Meneja wa Baby Madaha, Joe alithitisha
mipango hiyo na akasema sasa wanafanya kazi nyingi za muziki mpaka
zifike nyimbo 20 ambapo baada ya kuoana zitaanza kutoka mojamoja kwa
muda wa miaka minne.
“Ni kweli tumepanga kuoana, kikubwa ninaandaa nyimbo nyingi ili baada ya
ndoa nitasimama muziki na badala yake nitakuwa naachia nyimbo tu,”
alisema Baby anayetamba na Wimbo wa Nawaponda.
No comments:
Post a Comment